Jumamosi, 23 Novemba 2013

MWAKALEBELA AREJEA TFF



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametangaza wajumbe wa kamati ndogongo (standing committees) wakati zile za haki (judicial organs) na uchaguzi zitaundwa baadaye.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji kilichofanyika leo (Novemba 23 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Rais Malinzi alisema kamati hizo zimeundwa kwa mujibu wa katiba ili kuisaidia Kamati ya Utendaji.

Pia ametangaza wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji aliowateua. Wajumbe hao ni Richard Sinamtwa na Ramadhan Nassib, wakati wengine wanaoingia moja kwa moja kwenye Kamati ya Utendaji kutokana na kamati wanazoziongoza ni Dk. Paul Marealle na Saloum Umande Chama.

Kamati ya Fedha na Mipango inaongozwa na Makamu wa Rais wa TFF, Wallace Karia wakati wajumbe ni Francis Ndulane (Makamu Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammed, Geofrey Nyange, Kidao Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy na Cyprian Kuhyava.

Geofrey Nyange anaongoza Kamati ya Mashindano wakati wajumbe ni Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi, James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald ambi, Davis Mosha, Said George na Nassoro Idrissa.

Kinara wa Kamati ya Ufundi ni Kidao Wilfred wakati wajumbe ni Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedstus Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas Mihayo na Dk. Cyprian Maro.

Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana inaongozwa na Ayoub Nyenzi, Khalid Abdallah (Makamu Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya na Ibrahim Masoud.

Lina Kessy anaongoza Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake wakati wajumbe ni Shyrose Bhanji (Makamu Mwenyekiti), Zena Chande, Amima Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder, Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o na Engrid Kimaro.

Kamati ya Waamuzi inaongozwa na Saloum Umande Chama, Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor Mwandike, Soud Abdi na Zahra Mohamed.

Hamad Yahya Juma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi anaongoza Kamati ya Habari na Masoko wakati wajumbe ni Naibu Waziri January Makamba (Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla, Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji inaongozwa na Richard Sinaitwa, Moses Karuwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hanspoppe, Hussein Mwamba, Philemon Ntahilaja, Abdul Sauko na Imani Madega

Kiongozi wa Kamati ya Ukaguzi wa Fedha ni Ramadhan Nassib wakati wajumbe ni Zitto Kabwe (Makamu Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson, Goodluck Moshi, Golden Sanga na Elias Mwanjala. 

Dk. Paul Marealle anaongoza Kamati ya Tiba wakati wajumbe ni Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk. Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema na Asha Sadick.

RAGE AAGIZWA KUITISHA MKUTANO SIMBA


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.

Uamuzi wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

TFF itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.

Jumamosi, 16 Novemba 2013

NANI MWANASOKA BORA 2013 BARANI AFRIKA?


Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa orodha ya wachezaji 25 wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka huku Yaya Toure pamoja na Didier Drogba wakitumbukia ndani.

Kiungo wa Manchester City Yaya Toure ameshinda tuzo hiyo kwa miaka miwili mfululizo iliyopita na endapo atafanikiwa kutwaa ya mwaka huu atakuwa anaweka rekodi iliyowahi kuwekwa na nahodha wa Cameroon Samuel Etoo alishinda ya kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia 2002 hadi 2005.

Etoo ambaye anakipigia Chelsea kwa ujumla amewahi kutwaa tuzo hiyo mara nne lakini mwaka huu amejikuta akitupwa nje ya kinyang’anyiro hicho.

Ivory Coast imetoa wachezaji wawili kuwania tuzo hiyo ambao ni Gervinho na Didier Drogba wakati Nigeria wametumbukiza nyota watano John Obi Mikel.

Hafla ya kumtangaza mwanasoka bora wa Afrika wa mwaka 2013 inataraji kufanyika July 09 mwakani huko Lagos nchini Nigeria.
Nominees for African Footballer of the Year award:
Ahmed Musa (NGR/CSKA Moscow/RUS), Asamoah Gyan (GHA/Al Ain/UAE), Dame N'Doye (SEN/Lokomotiv Moscow/RUS), Didier Drogba (CIV/Galatasaray/TUR), Emmanuel Emenike (NGR/Fenerbahce/TUR), Islam Slimani (ALG/Sporting Lisbon/POR), John Obi Mikel (NGR/Chelsea/ENG), Jonathan Pitroipa (BUR/Rennes/FRA), Kevin Constant (GUI/AC Milan/ITA), Kwadwo Asamoah (GHA/Juventus/ITA), Luis Carlos Almada Soares 'Platini' (CPV/Omonia Nicosia/CYP), Mehdi Benatia (MAR/Roma/ITA), Mohamed Abou Trika (EGY/Al Ahly/EGY), Mohamed Salah (EGY/Basle/SUI), Nicolas Nkoulou (CAM/Marseille/FRA), Pierre-Emerick Aubameyang (GAB/Borussia Dortmund/GER), Ryan Mendes (CPV/Lille/FRA), Saladin Said (ETH/Wadi Degla/EGY), Seydou Keita (MAL/Dalian Aerbin/CHN), Sofiane Feghouli (ALG/Valencia/ESP), Sunday Mba (NGR/Warri Wolves/NGR), Victor Wanyama (KEN/Southampton/ENG), Vincent Enyeama (NGR/Lille/FRA), Gervinho (CIV/Roma/ITA), Yaya Toure (CIV/Manchester City/ENG)

RAMBIRAMBI MSIBA WA NYOTA COPA COCA-COLA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa Sayari, Fatuma Bahau ‘Crouch’ kilichotokea jana (Novemba 15 mwaka huu) kwenye Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
 
Msiba huo ni mkubwa katika mpira wa miguu kwani Fatuma ndiyo kwanza alikuwa anachipukia katika mpira wa miguu wa wanawake ambapo alikuwa mfungaji bora wa michuano ya U15 Copa Coca-Cola ya mwaka huu akichezea timu ya Ilala, hivyo mchango wake katika mchezo huu tutaukumbuka daima. 

Kwa mujibu wa mlezi wa mchezaji huyo, Stephania Kabumba, marehemu anasafirishwa kesho kwenda kwao Mwanza kwa ajili ya maziko ambapo kifo chake kimesababishwa na ugonjwa wa malaria. 
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Bahau, klabu ya Sayari, Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Kinondoni (KIFA) na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mungu aiweke roho ya marehemu Fatuma mahali pema peponi. Amina

MALINZI KUFUNGUA MICHUANO YA UHAI 2013


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atafungua rasmi michuano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 (U20) kwa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom mwaka huu.

Uzinduzi wa mashindano hayo utafanyika kesho (Novemba 17 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam saa 2 kamili asubuhi. Mechi ya ufunguzi itakuwa ya kundi A kati ya Azam na Coastal Union.  

Mechi nyingine za kesho ni kundi; Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Uwanja wa Karume), kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Uwanja wa Karume), Oljoro JKT na Simba (saa 10 jioni- Uwanja wa Karume).

Kundi C kutakuwa na mechi kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar itakayochezwa saa 2 kamili asubuhi kwenye Uwanja wa Azam Complex, na kwenye uwanja huo huo saa 10 jioni ni Rhino Rangers dhidi ya Tanzania Prisons.