Kocha mkuu wa timu ya taifa ya
Nigeria Stephen Keshi amesema kuwa kamwe hatokatishwa tamaa na maneno ya mashabiki
pamoja na wadau wa soka ambao wamekuwa wakimbeza juu ya maamuzi ya kikosi
chake.
Hajawahi kupoteza mbele ya wapinzani
wengine wa Afrika kwenye kipindi cha miaka mitatu lakini bado kocha huyo
anaonekana kujadiliwa zaidi kwa mabaya.
Lakini Keshi amekubali kuendana na
hali hiyo ya maisha huku akiamini kuwa ni sehemu ya maisha na siyo wote
watakaompenda.
Amesema hana wasi na hisia za watu
juu ya kazi na wala hajali jambo lolote lile kwakuwa familia yake inampenda na
inampa ushirikiano katika kufanya kibarua chake kwa ufanisi.
Nahodha huyo wa zamani wa The Super
Eagles ambaye alijiunga na kikosi cha Nigeria mwaka 2011, amefanikiwa kurejesha
hadhi ya soka la Nigeria kwa kufanikisha kutwaa kombe la mataifa ya Afrika
mwaka jana pamoja na kuiongoza nchi hiyo kuwa miongoni mwa mataifa mbalimbali
yatakayoshiriki fainali ya kombe la dunia mwaka huu wa 2014.
Licha ya mafanikio hayo, kwasasa
hatma ya kocha huyo imeanza kuweka walakini kufuatia baadhi ya vyombo vya
habari kuvujisha taarifa za ndazi za shirikisho la soka la Nigeria kuwa liko
mbioni kumuajiri kocha mpya raia wa kigeni.
Akifunguka kuhisiana na hatma ya
kibarua chake Keshi amesema kuwa kazi ya ukocha ni sawa na bahati nasibu ambayo
siku unapata na siku unakosa, cha msingi anajivunia kazi kubwa aliyoifanya kwa
kipindi chote alichoinoa timu hiyo na kama wataamua kumtumia na kumuajiri kocha
mwingine yeye yuko tayari na kamwe hawezi kuwa na kinyongo.
Aidha ameongezea kuwa kama watu
wameamua kuzungumza waache wazungumze na wala hawezi kuwazuia yeye ataendelea
kufanya yake ikiwemo kujiongezea sifa zaidi ya kuwa kocha pekee kutoka barani
Afrika kuyawezesha mataifa mawili kufuzu fainali ya kombe la dunia.
Kuelekea kwenye michuano ya kombe la
dunia ya mwaka huu Nigeria imeangukia kundi F linalojumuisha timu ya Iran, Bosnia-Hezrgovina
na Argentina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni