Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF
limeichagua April mosi mwaka huu kuwa ndiyo siku itakayofanyika zoezi la
upangaji wa makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika pamoja na ratiba ya
raundi ya pili ya 16 bora ya kombe la shirikisho.
Zoezi hilo kama kawaida litafanyika makao makuu ya
CAF yaliyopo Cairo nchini Misri ambapo raundi ya pili hatua ya awali ya makundi
ya klabu bingwa Afrika imepangwa kuchezwa kati ya March 28 hadi 30.
Kama ilivyoada zoezi hilo litaanzia na timu 8 ambazo
zimefuzu kwenye hatua ya makundi na timu za kombe la shirikisho barani Afrika.
Nikikumbushia matokeo ya mkondo wa kwanza ya 16 bora
mechi ambazo zilipigwa juma lililopita.
Mabingwa watetezi wa klabu bingwa Al Ahly ya Misri
ilianza kwa kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Al Ahly Benghazi ya Libya,
Zamalek ya Misri ilitoka sare ya kutofungana na Nkana fc ya Zambia wakati Sewe
Sport ya Ivory Coast ikiichapa TP Mzembe ya Congo DRC mabao 2-1.
Horoya fc ya Guinea ilikubali kipigo cha bao 1-0
dhidi ya Club Sportive ya Tunisia, Setif ya Algeria ikaichapa Coton Sport ya
Cameroon goli 1-0, Ac Leopards ya Congo ikaenda suluhu ya bao 1-1 na Al Hilal
ya Sudan wakati AS Vita ya Congo DRC ikiitandika Kaize Chiefs ya bondeni Afrika
kusini mabao 3-0.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni