Baada ya kikosi chake kushindwa
kuambilia alama tatu wakati wa mchezo wa hatua ya 16 bora klabu bingwa Afrika,
kocha mkuu wa Zamalek ya nchini Misri Ahmed Mido Hossam bado anaimani timu yake
inanafasi ya kusonga mbele kunako michuano hiyo.
Jumamosi iliyopita Zamalek ilijitupa
dimbani huko nchini Zambia kucheza dhidi ya wenyeji wao Nkana FC ukiwa ni
mchezo wa mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Afrika uliomalizika kwa
sare ya kutofungana.
Mido amekipongeza kikosi chake kuwa
kilicheza vizuri japo bahati haikuwa upande wao hivyo wanahitaji kutumia Baraka
ya uwanja wa nyumbani wa El Gouna kuhakikisha wanapata ushindi wakati wa mchezo
wao wa marudiano utakaopigwa mwishoni mwa juma hili.
Wakati huo huo Mido amewapongeza
wapinzani wao Nkana FC kuwa walionesha kiwango cha hali ya juu na walistahili
kupata ushindi lakini akatabahisha kuwa matokeo ya mchezo wa marudiano
wasitarajie kama watapata nafasi hata ya kufanya shambulizi langoni mwa Zamalek
kwakuwa wamejipanga kuhakikisha wanaumiliki mchezo kwa dakika zote 90.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni