Nahodha
wa timu ya taifa ya Ghana Asamoah Gyan amesisitiza kuwa ataendelea kuipigia
mikwaju ya penalty timu yake The Black Stars wakati wa matuta lakini si wakati
muhimu wa kuinusuru kubaki ama kuondolewa kwenye michuano ya kombe la dunia.
Nahodha huyo alishauriwa na marehemu mama yake kujihadhari na upigaji wa
penalty mara baada ya kutolewa kafara wakati akishindwa kuisaidia timu yake tutinga
fainali za AFCON mwaka uliopita.
Alikosa penalty muhimu kwenye mchezo wa ufunguzi wa nusu fainali ambao
walipokea kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Zambia tukio ambalo lilimpa wakati
mgumu kutokana na maneno ya mashabiki ambayo yalimfanya ajiondoe kwenye timu ya
taifa kwa muda.
Amesema kuwa kamwe hatarajii kujitolea kupiga mkwaju wowote wa penalty kwa
timu yake ila ikilazimika kupiga penalty ambayo haitakuwa na madhara ya kuiweka
kwenye wakati mgumu timu yake atapiga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni