Jumatano, 26 Machi 2014

ALGERIA SAYS IT CAN TAKE OVER 2017 AFCON

Kutokana na hali ya usalama kuwa bado haijatengamaa nchini Libya, Uongozi wa chama cha soka cha Algeria umejitokeza kutaka kuchukuwa nafasi ya kuandaa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 2017.

Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF bado halijafanya maamuzi, kama michuano hiyo ihamishwe kutoka Libya kupelekwa kwenye taifa lingine.

Waziri wa michezo wa Algeria Mohamed Tahmi amesema kuwa wapo tayari kuandaa fainali za AFCON kama Libya watapokonywa haki hiyo ya kuwa nchi mwenyeji kwa mwaka 2017.

Amesema kuwa nchi yake ina miundombinu ya kutosha na yakuridhisha kufana kwa fainali hizo na wanaamini wana uwezo wa kutosha wa kumudu mahitajio yote muhimu.

Aidha ameongezea kuwa wanasubiri maamuzi ya CAF kama watabaki na msimamo wa kuipa Libya haki hiyo ama laaa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni