Jumanne, 25 Machi 2014

2014 KAGAME CLUB CHAMPIONSHIP MOVED TO AUGUST



Michuano ya mwaka huu ya kombe la Kagame imesogezwa mbele hadi mwezi August badala ya mwezi June kama ilivyoarifiwa hapo awali ili kupisha kumalizika kwa michuano ya kombe la dunia itakayofanyika mwezi June huko Brazil.

Katibu mkuu wa baraza la vyama vya soka vya Afrika mashariki na kati Nicolaus Musonye amethibitisha kuhusiana na hilo na kutanabahisha kuwa bado hawajaipata nchi mwenyeji wa kuandaa michuano hiyo.
Amesema kuwa wapo katika mazungumzo na nchi za Rwanda na Sudan kuona uwezekano wa kuandaa michuano hiyo ambayo walipanga ifanyike mapema kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia lakini kutokana na timu nyingi kuwa bado wanakabiliwa na vibarua vya klabu bingwa pamoja na kombe la shirikisho barani Afrika wameamua kuyasogeza mbele hadi mwezi August.
Michuano hiyo ambayo inafadhiliwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame, kwa mwaka jana ilifanyika Darfur nchini Sudan na kushuhudiwa Vital’O kutoka Burundi ikitawazwa kuwa bingwa wakati timu kutoka nyumbani Tanzania Bara zikijiondoa kushiriki michuano hiyo kutokana na hali ya usalama ilivyo huko Sudan.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni