Jumatatu, 24 Machi 2014

JAHAZI KUZINDUA ALBAMU YAO YA 10 MWEZI MAY 2014

Kundi la Jahazi Modern Taarab chini ya Mkurugenzi wake mfalme Mzee Yusuph linataraji kuzindua albamu yake ya 10 mwezi May mwaka huu wa 2014.

Albamu hiyo ambayo imepewa jina la CHOZI LA MAMA LIKITOKA LINA LAANA KWA MWANA itajuisha nyimbo mbalimbali ambazo wamepewa wasanii tofauti akiwepo Prince Abubakar Soud Amigo, Mwasiti na wengineo.
Wimbo wa uliobeba jina la Album ameimba mwenyewe mfalme Mzee Yusuph na tayari umekamilika, wimbo ambao una maneno mazito ukisisitiza thamani ya mwanamke ama mama katika jamii.

Wimbo mwingine uliopo unaitwa Hasini hana sababu kaimba sauti ya Chiriku Bibie Khadija Yusupu, Aso kasoro hakuna kaimba Fatma Mahmoud Fatma Mcharuko.
Zipo nyimbo zingine kaimba Mwasiti, Amigo na Malkia Leila Rashid.
 
Akizungumza hapo jana wakati wa onesho lao la kila jumapili kwenye ukumbi wa Traventine Hotel Magomeni, wamesesma kuwa kadri siku zinavyozidi kwenda wataweka wazi ni tarahe ipi ya mwezi May na wapi uzinduzi huo utafanyika.

Aidha tayari Bi Harusi Rahma Machupa aliyeolewa mwishoni mwa juma lililopita amerejea kikosini ambapo sasa anajulikana kama mke halali wa Bwana Yusuph.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni