Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
litaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (TFF) kwa shughuli mbalimbili ikiwemo michezo na makongamano.
Kamati maalumu itaundwa kwa ajili ya kupanga na
kuratibu shughuli hiyo ambayo TFF imepanga kuadhimisha nchini nzima kwa kutumia
wanachama wake.
TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu
Tanzania (FAT) ilijiunga na FIFA Oktoba 8, 1964.
Wakati
huo huo: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo la Mnyanjani katika Jiji la
Tanga.
Hati hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75
Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6 ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu .
Kiwanja hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali,
kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa miguu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni