Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji
Yanga na Mbeya City lililofanyika jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam limeingiza sh. 175,285,000.
Watazamaji 30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi
hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo
iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati
kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh.
13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari
1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000
ambapo kila timu imepata sh. 11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika
kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh. 2,278,400.
Uwanja sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh.
3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,335,234.81.
Aidha:
Mshabiki mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi
bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Mbeya City
iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matei Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda
Kitunda, Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo
cha Polisi Chang’ombe akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo
asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini
hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa
hatua kwa mujibu wa sheria za nchini.
Tunatoa mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu
kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa.
Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni