Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi ametembelea Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi.
Katika ziara hiyo aliyoifanya jana (Februari 2 mwaka
huu), pia alikuwa mgeni rasmi mechi ya kugombea Kombe la Majaliwa kati ya Hull
City na Mbagala City, na kuahidi kuwa TFF itaandaa kozi za awali za ukocha na
uamuzi kwa Wilaya ya Ruangwa.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa mchezaji wa Vijana, Moro United na
Yanga, Omari Changa kilichotokea juzi (Februari 1 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu
kwani Changa wakati wake uwanjani akichezea timu mbalimbali alitoa mchango
mkubwa ambao tutaukumbuka daima.
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Changa,
klabu ya Moro United na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba
huo mzito.
Katika maziko TFF itawakilishwa na mjumbe wa Kamati
ya Utendaji, Kidao Wilfred, na imetoa rambirambi ya sh. 200,000.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni