Home For Everyone ATAKAYE NA AJEEEEE Facebook @Fatma Abdallah Chikawe Kichuna Twitter @FatmaChikawe Instagram @kichunafatma
Jumamosi, 8 Februari 2014
HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA JULIUS MTATIRO KWENYE UKURASA WAKE WA FACEBOOK
UTEUZI HUU NI ZAWADI KWA WATANZANIA;
Nimefurahi kusikia nami ni miongoni mwa watanzania wachache waliopendekezwa kushiriki katika Changamoto muhimu ya katiba ya nchi yetu.
Natambua kuna maelfu ya watanzania wenye uwezo mkubwa na sifa za kutosha kunishinda ambao walistahili, lakini nafasi nimepewa mimi.
Nakishukuru chama changu kwa kulipendekeza jina langu TCD ambako nao waliliwasilisha Ikulu hadi kupelekea uteuzi huu muhimu.
Namshukuru Rais na Watanzania wote kwa kunipa fursa hii.
Nimefurahi kusikia nami ni miongoni mwa watanzania wachache waliopendekezwa kushiriki katika Changamoto muhimu ya katiba ya nchi yetu.
Natambua kuna maelfu ya watanzania wenye uwezo mkubwa na sifa za kutosha kunishinda ambao walistahili, lakini nafasi nimepewa mimi.
Nakishukuru chama changu kwa kulipendekeza jina langu TCD ambako nao waliliwasilisha Ikulu hadi kupelekea uteuzi huu muhimu.
Namshukuru Rais na Watanzania wote kwa kunipa fursa hii.

Jambo moja la msingi ni kuwa "NITAKWENDA KATIKA BUNGE LA KATIBA KUTUNGA KATIBA YA WATANZANIA NA SIYO YA CHAMA CHANGU",
Kila hoja nitakayoisimamia lazima iwe na mvumo wa "......watanzania wanataka hili liwemo".
Hofu yangu kubwa ni kuwa, ikiwa tutaruhusu misimamo ya Vyama katika Bunge hili, ni chama chenye wabunge wengi ndiyo kitatoa katiba, na makundi mengine yenye wabunge wachache na hoja za msingi,yatadharauliwa na hoja kutupwa mbali.
Mungu Ibariki Tanzania.
JUDICIAL ORGANS, INDEPENDENT & STANDING COMMITTEES TFF
BOARD OF TRUSTEES; Said
Hamad El-Maamry, Stephen Mashishanga, Dr Ramadhan Dau, Joel Bendera, Mohamed
Abdul Aziz
Kamati ya Nidhamu;
Tarimba Abbas (Mwenyekiti), Advocate Jerome Msemwa (Makamu Mwenyekiti), Kassim
Dau, Nassoro Duduma, Kitwana Manara.
Kamati ya Rufani ya Nidhamu; Profesa Mgongo Fimbo (Mwenyekiti), Advocate Hamidu
Mbwezeleni (Makamu Mwenyekiti), Titus Bandawe, Twaha Mtengera, Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) mstaafu Boniface Mpaze.
Kamati ya Maadili;
William Erio (Mwenyekiti), Advocate Ezekiel Maganja (Makamu Mwenyekiti),
Advocate Victoria Mandari, Kanali mstaafu Enos Mfuru na Said Mtanda.
Kamati ya Rufani ya Maadili; Jaji mstaafu Stephen Ihema (Mwenyekiti), Wakili Alesia
Mbuya (Makamu Mwenyekiti), Lilian Kitomari, Jabir Shekimweri na Chabanga Hassan
Dyamwale.
Kamati ya Uchaguzi;
Advocate Melchesedeck Lutema (Mwenyekiti), Advocate Walter Chipeta (Makamu
Mwenyekiti), Hamidu Mahmoud Omar, Jeremiah John Wambura, Hassan Dalali.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi; Advocate Julius Lugaziya (Mwenyekiti), Advocate Mwita
Waissaka (Makamu Mwenyekiti), Juma Abeid Khamis, Rashid Dilunga, Masoud
Issangu.
Kamati ya Fedha na Mipango; Wallace Karia (Mwenyekiti), Francis Ndulane (Makamu
Mwenyekiti), Omari Walii, Eliud Mvella, Said Muhammad, Geofrey Nyange, Kidao
Wilfred, Ayoub Nyenzi, Lina Kessy, Cyprian Kuhyava.
Kamati ya Mashindano;
Geofrey Nyange (Mwenyekiti), Clement Sanga (Makamu Mwenyekiti), Msafiri Mgoyi,
James Mhagama, Mohamed Nassoro, Moses Katabaro, Seif Ahmed, Gerald Ambi, Davis
Mosha, Said George, Nassoro Idrissa (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius
Rutayuga).
Kamati ya Ufundi;
Kidao Wilfred (Mwenyekiti), Athumani Kambi (Makamu Mwenyekiti), Vedastus
Lufano, Blassy Kiondo, Rahim Kangezi, Patrick Kahemele, Daud Yassin, Nicholas
Mihayo, Dk. Cyprian Maro (Mshauri wa Rais Ufundi- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana; Ayoub Nyenzi (Mwenyekiti), Khalid Abdallah (Makamu
Mwenyekiti), Ali Mayay, Mulamu Ng’hambi, Apollo Kayungi, Said Tully, Luteni
Kanali Charles Mbuge, Lameck Nyambaya, Ibrahim Masoud (Mshauri wa Ufundi wa
Rais- Pelegrinius Rutayuga).
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake; Lina Kessy (Mwenyekiti), Shyrose Bhanji (Makamu
Mwenyekiti), Zena Chande, Amina Karuma, Dk. Cecilia Makafu, Zafarani Damoder,
Beatrice Mgaya, Sofia Tigalyoma, Martin Mung’ong’o, Ingridy Kimaro.
Kamati ya Waamuzi;
Saloum Umande Chama (Mwenyekiti), Nassoro Said (Makamu Mwenyekiti), Charles
Ndagala (Katibu), Riziki Majala, Kanali Isaro Chacha, Paschal Chiganga, Victor
Mwandike, Soud Abdi, Zahra Mohamed.
Kamati ya Habari na Masoko; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Naibu Waziri January Makamba
(Makamu Mwenyekiti), Tido Mhando, Yusuf Manji, Yusuf Bakhresa, Samwel Nyalla,
Jack Gotham, Fredrick Mwakalebela, Juma Pinto.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji; Advocate Richard Sinamtwa (Mwenyekiti), Advocate Moses
Kaluwa (Makamu Mwenyekiti), Zacharia Hans Poppe, Hussein Mwamba, Philemon
Ntahilaja, Abdul Sauko, Imani Madega.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha; Ramadhan Nassib (Mwenyekiti), Zitto Kabwe (Makamu
Mwenyekiti), Nicholas Magarinza, Jackson Songora, Epaphra Swai, Kalilo Samson,
Goodluck Moshi, Golden Sanga, Elias Mwanjala.
Kamati ya Tiba;
Dk. Paul Marealle (Mwenyekiti), Dk. Fred Limbanga (Makamu Mwenyekiti), Dk.
Mwanandi Mwankemwa, Dk. Nassoro Matuzya, Dk. Eliezer Ndelema, Asha Sadick.
Kamati ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni; Ahmed Idd Mgoyi (Mwenyekiti), Shaffih Kajuna Dauda (Makamu
Mwenyekiti), Boniface Pawasa, Deo Lucas, Juma Mgunda, John Kanakamfumu, John
Mwansasu.
AD HOC COMMITTEES
Kamati ya Kutathimini Muundo wa Ligi; Dk. Mshindo Msolla (Mwenyekiti), Idd Mshangama
(Katibu), Rahim Kangezi, Amri Said, Sunday Manara, Salim Bawazir, Lucas Kisasa.
Kamati ya Kutathimini Muundo wa Bodi
ya Ligi; David Nchimbi (Mwenyekiti), Edwin
Kidifu, Jones Paul, Evans Aveva, John Jambele, Masoud Sanani, Pelegrinius
Rutayuga.
Jumatatu, 3 Februari 2014
TFF YAADHIMISHA MIAKA 50 FIFA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
litaadhimisha miaka 50 tangu lipate uanachama wa Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (TFF) kwa shughuli mbalimbili ikiwemo michezo na makongamano.
Kamati maalumu itaundwa kwa ajili ya kupanga na
kuratibu shughuli hiyo ambayo TFF imepanga kuadhimisha nchini nzima kwa kutumia
wanachama wake.
TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu
Tanzania (FAT) ilijiunga na FIFA Oktoba 8, 1964.
Wakati
huo huo: Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
limepata hati ya kiwanja chake kilichopo eneo la Mnyanjani katika Jiji la
Tanga.
Hati hiyo ya miaka 99 ya kiwanja hicho namba 75
Block D chenye ukubwa wa ekari 7.6 ilikabidhiwa kwa TFF, Januari 13 mwaka huu .
Kiwanja hicho kitaendelezwa kwa matumizi mbalimbali,
kubwa ikiwa ni uwanja wa mpira wa miguu.
PAMBANO LA YANGA, MBEYA CITY LAINGIZA MIL 175
Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji
Yanga na Mbeya City lililofanyika jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam limeingiza sh. 175,285,000.
Watazamaji 30,411 walikata tiketi kushuhudia mechi
hiyo kwa viingilio sh. 5,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 kwa VIP A. Yanga ndiyo
iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0.
Mgawanyo wa mapato ulikuwa Kodi ya Ongezeko la
Thamani (VAT) sh. 26,738,389.83, gharama za kuchapa tiketi sh. 2,919,200 wakati
kila klabu ilipata sh. 42,960,086.50.
Uwanja sh. 21,844,111.53, gharama za mechi sh.
13,106,466.92, Bodi ya Ligi sh. 13,106,466.92, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 6,553,233.46 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 5,096,959.36.
Nayo mechi ya Simba na Oljoro JKT iliyochezwa Februari
1 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 47,705,000
ambapo kila timu imepata sh. 11,254,122 kutokana na watazamaji 8,267.
Mgawanyo mwingine katika mechi hiyo iliyomalizika
kwa Simba kushinda mabao 4-0 ni Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh.
7,277,033.90 na gharama za kuchapa tiketi sh. 2,278,400.
Uwanja sh. 5,722,434.92, gharama za mechi sh.
3,433,460.95, Bodi ya Ligi sh. 3,433,460.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 1,716,730.47 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,335,234.81.
Aidha:
Mshabiki mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi akidaiwa kukutwa na tiketi
bandia kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Mbeya City
iliyochezwa jana (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matei Cosmas (28) ambaye ni mkazi wa Buza Njiapanda
Kitunda, Dar es Salaam amefunguliwa jalada namba CHA/IR/900/2014 kwenye Kituo
cha Polisi Chang’ombe akidaiwa kupatikana na tiketi bandia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo
asubuhi (Februari 3 mwaka huu) limeamkia Kituo cha Polisi Chang’ombe kusaini
hati ya maelezo dhidi ya mtuhumiwa.
Ni imani ya Shirikisho kuwa mtuhumiwa atachukuliwa
hatua kwa mujibu wa sheria za nchini.
Tunatoa mwito kwa washabiki wa mpira wa miguu
kuepuka kununua tiketi kutoka mikononi mwa watu, kwani kufanya hivyo ni kosa.
Tiketi zinauzwa kwenye sehemu maalumu zenye chapa ya TFF.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)