Alhamisi, 5 Desemba 2013

SAMATTA OUT TUZO ZA CAF




Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa orodha ya mwisho ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mwanasoka bora Afrika na na wengine watano wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anaekipigia ndani ya bara hilo.

Majina ya wachezaji 10 wanaowania tuzo ya mwanasoka bora ni Mohammed Abutrika kutoka Misri, Pierre Emerick Ubamiyang kutoka Gabon, Didier Drogba na Yaya Toure kutoka Ivory Coast, Emmanuel Emenike, Vicent Enyima, Ahmed Mussa na John Mikel Obi wote kutoka Nigeria, Asamoh Gyan kutoka Ghana na Jonathan Pitroipa kutoka Burkina Faso.

Katika orodha ya wachezaji Watano wanaokipigia ndani ya Afrika Mohammed Abutrika ametinga kwa mara nyingine huku mshambuliaji kutoka nyumbani Tanzania anaekipigia ndani ya TP Mazembe ya Congo Mbwana Ally Samatta ametupwa nje ya kinyang’anyiro na nafasi yake imechukuliwa na Rainford Kalaba pamoja na Tresor Mputu kutoka kwenye klabu ya TP Mazembe huku Nigeria ikipata muwakilishi mmoja ambaye ni Sunday Mba.

Hafla ya utoaji Tuzo itafanyika January 9 mwakani huko Lagos nchini Nigeria.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni